Hospitali ya wilaya ya korogwe [Makuyuni] imebahatika kupokea huduma mkoba [tembezi] ya madaktari bingwa wa Mama Samia. Huduma hizo zinatolewa kwa siku tano kuanzia tarehe 12/05/2025 hadi tarehe 17/05/2025, ambapo zoezi rasmi limeanza leo siku ya jumanne kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Madaktari wanaoshughulika na kutoa huduma hizo wametoka sehemu mbalimbali nchini Tanzania kwa lengo la kuhakikisha huduma bora za afya na za kibingwa zinawafikia watu wa hali ya chini. Huduma hizi zinatolewa kama moja ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.Huduma zinazotolewa ni kama vile;-
Kutokana na watu wa hali za chini kushindwa kuzifikia huduma za madaktari bingwa nchini, hivyo basi serikali ya awamu ya sita imeanzisha kampeni hii ya huduma mkoba (tembezi) lengo kubwa ni kuwarahisishia watu hawa kupata huduma hizo kwa urahisi kulingana na hali zao. Pia kampeni hii imeanzishwa kama hamasa ya kuwafikia watu wa ngazi ya chini kwenye mahitaji yao ya kimsingi kama vile afya, elimu na huduma nyingine
Huduma zinatolewa kwa utaratibu wa kawaida yani mwenye bima atahudumiwa kwa kutumia bima yake na asie na bima atalazimika kutumia gharama za matibabu na ambao wanahudumiwa bure kisheria basi watahudumiwa. Ujaji wa madaktari na uwepo wao siku zote hospitalini gharama ni za serikali, hii inaonesha ni kwa kiasi gani serikali ya awamu ya sita inawajali na kuwathamini wananchi wake wa hali zote nchini.
Licha ya hali ya hewa ya mawingu na manyunyu wananchi wa wilaya ya korogwe vijijini wamejitokeza kwa wingi mno, hii inaonesha ni kwa jinsi gani wana uhitaji wa dhati wa kupata huduma hizo za kibingwa. Pia wananchi wameshukuru sana kufikiwa na huduma hizi maana ilikuwa inawagharimu kuandaa gharama kubwa mpaka kuzifikia huduma hizo ambapo hali hii inapelekea wagonjwa hao kuishi na magonjwa yao mtaani kutokana na hali zao za kimaisha, hivyo wanashukuru na wanaomba huduma hizi zipatikane kila baada ya muda fulani ili kupunguza vifo vya watu wa ngazi za chini ili kulinda rasilimali watu na Taifa kwa ujumla
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki miliki©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa