Vikundi 13 vya wajasiliamali katika halmashauri ya Wilaya ya Korogwe wapata mafunzo ya matumizi bora ya Mkopo wa asilimia 10.Mafunzo hayo yameanza leo tarehe 14.01.2025 ambapo yatadumu kwa muda wa siku mbili kabla ya kupatiwa mikopo hiyo.
Aidha katika mafunzo wanavikundi wamesisitizwa kuwa waaminifu ili kufanikisha kurudisha mikopo hiyo kwa wakati na kuwa na ushirikiano kwa wataalamu wa Halmashauri pindi wanapofuatilia maendeleo ya vikundi hivyo.
Wawakilishi wa vikundi wamesema wanaishukuru serikali ya awamu ya sita na Hamashauri ya Wilaya ya Korogwe kwa kuandaa mafunzo hayo ili kuweza kupata uwanda mpana wa namna ya kufanya matumizi bora ya mikopo hiyo ili kuendesha vikundi vyao kwa weledi na kufikia malengo ambayo wamejiwekea kwenye vikundi.
Korogwe District Council
Postal Address: P.o Box 584
Telephone: 027- 2650017/2650061
Mobile:
Email: ded@korogwedc.go.tz
Haki milikiĀ©2016 KDC Haki zote zimehifadhiwa